Matumizi ya kitunguu saumu angalau kwa siku 5 kwa wiki kunaongeza ubora na urefu wa maisha sawa nakuongeza kiasi cha mwaka mmoja kwenye maisha yako ukilinganisha na ambao hawatumii.
Hii inatokana na ukweli kwamba, kitunguu saumu ni kinara kwenye afya ya moyo na kukinga saratani hasa saratani ya tumbo.
👉Kwenye afya ya moyo
• Inaboresha utendaji kazi wa arteri. Unajua afya ya ateri ndio afya yako. Zikichakaa ndivyo na wewe unazeeka hata kama ni kijana
• Vinapunguza kasi ya artherosclerosis – hii ni hali ambayo mishipa ya damu hasa ile mikubwa inapungua ukubwa kwa sababu ya mafuta. Na hivyo damu kushindwa kufika kwa kiasi kinachotosha kwenye viungo vya mwili.
• Vinashusha kolestro
Huhitaji kunywa nyingi sana…
Kiasi cha ¼ kijiko cha chai = 800mg (sawa punji 1 tu ya kitunguu saumu).
Ikiwa unatumia kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo tumia mara mbili kwa siku.
Baada ya miezi 3 utendaji kazi wa arteri zako utakuwa umeongezeka kwa asilimia 50.
Faida nyingine za kitunguu saumu
• Inaongeza radha ya chakula
Wako Dr.Penina.

0 Comments